Historia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi:1
Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh ndugu zangu katika Iymaan,hakika leo ni siku nyingine tunakutana katika ukurasa wetu kama ilivyo ada kujuzana mambo mbalimbali yahusuyo Dini yetu Adhwiim ya UISLAAM,na leo hii kwa Idhin ALLAH tutaangalia Historia ya Mjumbe wa mwisho wa ALLAH kipenzi cha ALLAH, Kiigizo chema kwetu Mtume Muhammad(S.A.W),naamu twendeni pamoja In Sha Allah.
"FIKISHA YALIYOFIKISHWA"
"Wa azah Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh"
- Mtume Muhammad(S.A.W) alizaliwa Makka-Arabuni tareh 12-Rabbil Awwal(Mfungo sita) Miaka 54 BK.Sawa na 20(04) 570/571.B.I,Juma Tatu Alfajiri.Ndugu zangu kwenye swala la mwaka wa kuzaliwa kwake hapa kuna Maulamaa wametofautiana na ndiyo maana nimeweka miaka yoote miwili hapo.
"Na sema ukweli umefika nauongo umetowekw/utaondoka,kwa hakkika uongo ni wenye kuondoka"( QUR'AN.17:81).
- Baba yake alikuwa akiitwa Abdallah(ikiwa na maana ya mja wa ALLAH) na alifariki miezi 6 kabla ya kuzaliwa kwa mwanae Muhammad,na Mama yake anaitwa Amina(mwenye Iymaan/kuamini) nae alifarika kabla ya Mtume kufikisha miaka 6, hapo alilelewa na Babu yake Abdul Muttalib naye alifariki miaka miwili baadae na baada ya hapo alilelewa na Ami yake(Baba Mdogo) aitwae Abu Taliib.Kwa ufafanuzi huu basi tunaona kuwa Mtume Muhammad alikuwa Yatima toka utotoni kwake.Mtume Muhammad alinyonyweshwa maziwa ya mwanamke wa Maskini aitwae Halima kwa miaka 2 baada ya yeye kukataa kunyonya maziwa ya mamae alipozaliwa,hii ilikuwa na maana kwamba yeye amekuja kuwa mtetezi wa watu wote si maskini si matajiri.
- Anatokea katika ukoo wa Banu Hashim wa kabila la QURAISH, na baada ya kuwa kijana wa makamo alikuwa akifanya biashara akimsaidia Ami yake Abu Taliib,alikuwa akisafiri mara kwa mara kwenda Sham na Baba yake Mdogo,pia alikuwa anachunga kondoo,lakini pia Mtume wetu Habib alikuwa anatengeneza viatu na nguo zake mwenyewe na hivyo kumfanya awe tofauti na vijana wengine wa Makka huku akijazwa Ustaarabu na Khekima.
"FIKISHA YALIYOFIKISHWA"
"Wa azah Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh"
Comments
Post a Comment