Histotia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi :6
Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh ndugu zangu katika Iymaan,naam Alhmadulillah kwa kuwa tunakutana tena leo hii kwenye muendelezo wa Historia ya Mtume Muhammad kwa uchache wake na tukiwa mwishoni mwa Mada yetu.
BISMILLAH RAHMAN RAHIIM.
BISMILLAH RAHMAN RAHIIM.
MAPOKEZI YA MTUME MUHAMMAD NA ABU BAKAR SIDIQ KATIKA JAMII YA MADINA BAADA YA KUWASILI KWAO.
Mtume Muhammad na Abu Bakar walipowasili Madina walipokelewa kwa shangwe na furaha na Waislam wa Madina kwani walikuwa na hamu kubwa ya kumuona Mtume wa Mwenyezi Mungu.
Mtume Muhammad baada ya kufika Madina alimuachia Ngamia wake (HATAMU) ambae alikuwa anamtumia katika usafiri, na Ngamia huyu alienda kusimama katika kiwanja tupu cha ndugu wawili Mayatima na kuanza kula majani, na Mtume Muhammad aliamua kununua kiwanja kile na kujenga Msikiti na nyumba ndogo ya pembeni.
Baadae Msikiti huu pamoja na nyumba ile vilikuwa sehemu ya kufikia wegeni(wasafiri) wasiokuwa na mahali pa kufikia, pia ilikuwa ni sehemu ya mikutano ili kujadili matatizo ya Jamii.
Kwa kuwa wafuasi wengi wa Mtume Muhammad waliotoka Makka(MUHAJILINA) waliacha mali zao huko hivyo iliwalazimu Waislam wa Madina (ANSAR) kuwasaidia,na waislam wa Madina walitowa kila walichonacho ili kuwasitiri waislam wenzao waliotoka Makka na ilifikia hatua hadi Waislam wanaume wa Madina waliamua kuwaacha baadhi ya wake zao ili waislam wa Makka waweze kuwaoa.
Mtume Muhammad alipokuwa Makka alikuwa akipata Wahyi kutoka kwa MWENYEZI MUNGU kuhusiana na IYMAAN&ITIKADI, na hii ilikuwa na lengo la kuthibitsha Iymaan na kupinga shirki,LAKINI Madina alipokea Wahyi kuhusiana na;.Vyakula,Vinywaji,Ndoa na Maisha ya kikoo na kijamii,Akhlaki,BiasharanAmani,Uhalifu na Adhaba zake.
Mwaka wa pili baada ya Hijra, Jeshi la kikureishi la watu elfu 1000 lilijizatiti barabara kwa silaha na kuanza safari ya kuelekea Madina, waislam wa Madina nao waliposikia habari hizi waliunda jeshi la watu 300 na kwenda kukabiliana nao na Vita hii ilipigwana eneo liitwalo BADRI,na ndiyo maana vita hii inaitwa vita ya BADRI.Licha ya uchache wa waislamu wa Madina lakini walishinda vita hii.
TAKWIMU/KALENDA YA KIISLAM.
Takwimu ama Kalenda ya kiislam ilianza kuhesabiwa toka Mtume Muhammad(S.A.W) aamie Madina ambayo ni Tarehe1/Muharam/wa Hijra AU Ta: 15/07/622 B.I.
Tukutane siku nyingine kwa kumalizia Historia hii mzuri ya Mtume Muhammad(S.W.A).
"FIKISHA YALIYOFIKISHWA"
Wa azah Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh"
Comments
Post a Comment