Nguzo [5] za Uislam.
Aslaam 'Akaykum warahmatullah wabarakatuh ndugu zangu katika Iymaan naam baada ya mda mrefu pia leo twakutana tena ili kujuzana ama kukumbushana hili na lile kuhusu Dini yetu adhwim ya Uislam Dini ya haki.Kama vile tunavojua kuwa sie waja wa Allah hatujakamilika na ni wenye kusahau hivyo ni jukum la kila mmoja wetu kumkumbusha mwenzake. Na leo hii tutaangalia Nguzo [5] kuu z Uislam ambazo kwamba endapo tukishikamana nazo ki ukweli ukweli wa Moyo basi tutakuwa waislam kamili na Allah ataturidhia na Radhi zake tutaanza kuziona hapa hapa Duniani kabla ya kesho Akhera,Hivyo basi tuanze hapa. Kalmat Tawheed/Shahada Ina maana kwamba ni kushuhudia kwa Allah peke yake na si viumbe vingine na kuamini kuwa Muhamamad ni Mtume wake .[Ashahad Llah ilaha ila ALLAH wa ashahad anna Muhammad Rassulullah] Ndugu zangu Shahada ndiyo nguzo ya kwanza ya Uislam ndiyo mana inatajwa kwenye kila kitu kinachohusiana na Uislam kama vile kwenye Swala,Dua'a hata mtu an...