Historia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi :7

Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh ndugu zangu katika Iymaan naam baada ya Muda mrefu wa kukaa kimya hakika leo tunaendelea kujuzana na tukiwa mwisho kabisa wa Historia ya Mtume Muhammad(S.A.W),na kabla ya yote niwaombe radhi ndugu zangu maana nakaa kimya kwa mda mwingi lakini In Sha ALLAH Allah ataweka wepesi .Na leo tutaangalia kuanzai  Hija ya Mtume Muhammad(S.A.W) hadi kifo chake ambapo ndiyo mwisho wa Historia yetu,

BISMILLAH RAHMAN RAHEEM.

HIJA YA KUAGA BAADA YA KURUDI MAKKA.

Mtume Muhammad kafanya Hijja yake katika mwaka wa 10 baada ya Hijra(10 B.H) na ijapokuwa toka aanze ujumbe wake haikufika Miaka 24,lakini kulikuwepo Waislamu 114,000 waliofutana naye kwenda Makka.Kwa hakika mwengine aliyepata ushindi  mkubwa kama huuu, kwani tukianza Mika 11 nyuma  tunamuona Mtume  akitolewa Makka na kusakwa kutaka kuuliwa na leo ni kiongozi bor a wa Arab na Dunia ya Waislam kwa ujumla.

Khutba ya mwisho aliyoitoa Mtume Muhammad(S.A.W) katika mnasaba huu wa Hajj ilikuwa ni kutimiza ujumbe wake,kuja kwa siku ya malipo,kuwaheshimu Wanawake na utakatifu wa mali na uhai.

AKASEMA "Jueni Waislam wote ni ndugu na kwa kuwa sote ni ndugu, moja nimekuachieni kitu ambacho mkishikamana nacho hamuwezi kupotea,ni Kitabu cha ALLAH(QUR'AN) na mafundisho ya Mtumewe (Sunna zake)"Wakati huu ndipo alipoteremshiwa Aya ya mwisho kabisa takriban kutoka kwa Mola wake.

         "Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na kukutimizieni neema yangu,na nimekupendeleeni  Uislam uwe Dini yenu"(Q:5:3)

KUFA KWA MTUME MUHAMMAD(S.A.W)
Mtume Muhammad hakukaa sana baada ya kupata Wahyi wa mwisho, akawa mgonjwa na baada ya kupata uzima kidogo,alianza kudhoofu tena na nguvu zake kumwishia,Mchana wa Juma Tatu tareh 12 Rabil-Awwal mwaka wa11 baada ya Hijra(Tarehe 8/6/632 B.I,wakati Mtume alipokuwa akimuomba Mola kwa Moyo wake wote; roho yake takatifu akitoka kwenda kwa Rafiki yake alije juu(ALIFARIKI)

"Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea(Q:2:156)
Watu wa Madina waliingiwa na huzuni mkubwa sana,Umar Sahaba mkubwa wa Mtume Muhammad hakutaka kusadiki kuwa Mtume amefariki na hivyo alikwenda Msikitini ambako watu walikusnayika kumuombea Mungu Mtume wao akatangaza akasema "Nitamuua yeyote mwenye kusema Mtume amekufa "Na kwa kuwa Umar alikuwa karibi sana na ni mtu muhima sana kwa Mtume.Waislam waliingiwa na Khofu na kukaanza fujo na mbabaiko wa hapa na pale hadi Abu Bakar alipopanda Mimbari na kusema.
 "Ikiwa mkimuabudu Muhammad basi keshafariki,ikiwa mkimuabudu ALLAH basi yu hai.

Na huu ndiyo ulikuwa mwisho wa Maisha ya Mtume Muhammad hapa Duniani,Nduga zangu katika Iymaan jukumu letu kubwa tulilo nalo ni kushikamana na yale ALLAH anayoyahitaji na kukatazika na makatazo yake kupitia mafundisho ya Mtume Muhammad(S.A.W).

NB :Historia hii nimeitoa kwenye kitabu kiitwacho "MAFUNZO YA KIISLAM KWA MAWASILIANO"Cha International Isalmic Federation of Students Organization(I.I.F.S.O)

Ahsanteni sana na tukutane kwenye Mafundisho mengine mazuri yajayo.

"FIKISHA YALIYOFIKISHWA"

"Wa azah Aslaam 'Alaykum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh"


Comments

Popular posts from this blog

Mitume 25 iliyotajwa kwenye QUR'AN.

Historia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi:1

Histotia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi :6