Nguzo [5] za Uislam.
Aslaam 'Akaykum warahmatullah wabarakatuh ndugu zangu katika Iymaan naam baada ya mda mrefu pia leo twakutana tena ili kujuzana ama kukumbushana hili na lile kuhusu Dini yetu adhwim ya Uislam Dini ya haki.Kama vile tunavojua kuwa sie waja wa Allah hatujakamilika na ni wenye kusahau hivyo ni jukum la kila mmoja wetu kumkumbusha mwenzake.
Na leo hii tutaangalia Nguzo [5] kuu z Uislam ambazo kwamba endapo tukishikamana nazo ki ukweli ukweli wa Moyo basi tutakuwa waislam kamili na Allah ataturidhia na Radhi zake tutaanza kuziona hapa hapa Duniani kabla ya kesho Akhera,Hivyo basi tuanze hapa.
- Kalmat Tawheed/Shahada
Ina maana kwamba ni kushuhudia kwa Allah peke yake na si viumbe vingine na kuamini kuwa Muhamamad ni Mtume wake.[Ashahad Llah ilaha ila ALLAH wa ashahad anna Muhammad Rassulullah]Ndugu zangu Shahada ndiyo nguzo ya kwanza ya Uislam ndiyo mana inatajwa kwenye kila kitu kinachohusiana na Uislam kama vile kwenye Swala,Dua'a hata mtu anaposilimishwa basi anatamkishwa shahada tu kwa ridha yake anakuwa taari ni Muislam,na Mtume Mhammad(S.A.W) anatuambia yule ataetamka shahada wakati wa mauti yake basi Pepo ni halali yake.Hii inaonesha ukubwa na hadhi ya shahada kwa waislam na ni moja kati ya vitu vinavyo tutofautisha sisi na wasio Waislam.Hivyo tumuombe Allah atuja'alie kujua ukubwa wa shahada hii zaidi na zaidi.
2.Iqamat Swalaa.
Kiswahili rahisi cha sentensi ni kushikama na swala,kushikamana na swala maana yake ni kuswali swala{5}ambazo ni Faradhi kwa kila muislam na zile za Sunna.Kwenye hili pia ni jambo muhimu zaidi na zaidi,bi maana kwamba hata ukiwa unatenda A'amali njema kwa kiasi kikubwa sana lakini bila swala sawa na hakuna,na ndiyo tunaambiwa wa sio Waislam wakitenda mema basi watapata Rehma za Duiani hapa hapa tu siku ya Qiyama hawatakua na chao.Hivyo tujibidihishe kwa nguvu zetu zote kuswali swala[5]za Faradhiwi na za Sunna ili tufikie lengo la uchamungu.
3.Itaw Dhakaa.
Hii ina maana ya kutoa Dhakaa/Sadka pia. Dhakaa hutolewa mara moja kila mwaka kwa Muislam ambayo ni katika kipindi cha Eid El-Hajj na sadaka ni za kila siku,na kwenye sadaka hapa ikumbukwe kuwa si kutoa pesa au mali tu kwa wasiojiweza na watoto, pia hata matendo mema lugha safi kwa waja wengine pia ni kati ya sadaka.na tunaambiwa siku ya Qiyama itafika mda ALLAH ataamrisha mtu aangaliwe kama aliwai toa sadaka basi atawekewa kwenye mema yake na uzito ukizidi basi pepo ni makazi yake.Je ndugu zangu mimi na wewe hatuhitaji pepo kweli hakika tunahitaji basi tujibidihishe kufanya yalo mazuri na tuepuke yalo mabaya.
4.Saum Ramadhaan.
Na hakika ndiyo mwezi ambao tuko nao, Kufunga Ranadhaan ni Faradhi[wajibu] kwakila Muislam aliyefikia Umri wa Balehe ambaye hana kinachomzuia kama vile Maradhwi au hali ya kuichumi.Na kufunga Ramadhaan kuna fadhila nyingi sana kama vile kukubaliwa Dua'a,Kusamehewa Madhambi N.K.
5.Hijjun Baytun Liman Stat'wa.
Kuhiji Makka kwa mwenye uwezo,ina maana kwamba kwa ambaye ana uwezo ambao una chumo la halali ndani yake basi na aende Kuhiji hata mara moja katika umri wake wa Duniani.Lakini Hijja hii inabidi mmoja wetu anapokwenda kuhiji basi familiya yake iridhiye na asihiache katika hali ya dhiki.Na mwenye kufanya hivi Hijja yake haitakubaliwa.Mtume Muhammad(S.A.W)alienda Hajj mara moja katika Umri wake wa Duniani ila kwa sie Umma wake kama mtu una wezo wa chumo halali basi unaweza kwenda kwa kadri ya uwezavyo.
Na hapa ndiyo mwisho wa Mada yetu kwa leo.Ndugu zangu hakika ili Mtu ufukie lengo la Uislam basi lazima tushikamane na Nguzo hizi [5] za Dini yetu a sivyo basi tutakuwa nunsu nusu,na pia kama nilivyosema siku ya Qiyama itafika muda Mtu ataangaliwa Swala za Sunna,Funga ya Ramadhan au Sunna,ataangaliwa pia kama alikuwa anatoa sadaka na vingine vingi na mwenye kukutwa navyo hivi basi pepo ni makazi yake halali.Na tumuombe ALLAH atuja'alie Fikra za kutenda haya kwa ajili yake ili tupate kuiona Janna..Nilipokosea basi ALLAH anisameh maana nami ni Mja wake na sijakamilika na anipe ufaham sahihi zaidi ili tuendelee kujuzana In Sha ALLAH. ALLAHU AALAM.
"FIKISHA YALIYOFIKISHWA"
"Aslaam 'Alaykum warahmatullah wabarakatuh"
Comments
Post a Comment