Buthula'anul Wudhuu(Yanayotengua Udhu).
Aslaam Alaykum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh ndugu zangu katika Imaan, kwanza tumshukuru ALLAH(S.W) kwa kutuchagua kuwa miongoni mwa waja wake wenye kuiona leo hii tukiwa na Afya swafi maana kuna wengi wanaohitaji kuwa kama sisi lakini Allah kawaja'alia Mtihani,tuseme In Sha Allah ALLAH awaja'alie Tawfiq,kwa hiyo tulo wazima basi tumshukuru ALLAH kwa uchache wa shukran kwa kusema ALHAMDULILLAH.
Leo Bi Idhin Llah In Sha Allah tutaangalia Mambo(5) ambayo kwamba yanatengua Udhu kwa Mtu na kumfanya asiwe na Rukhsa ya ALLAH kuiendea SWALA.Twendeni pamoja.
kwa maana ya kisharia(Dini) ni ibada ya kabla ya swala na baada ya twahara ambayo huambatinisha utiaji /uwekaji maji kwenye viungo vya mwili pamojana Dua.
Ndugu zangu Udhu ni jambo la kuzingatia sana maana hata Swawabu za swala zetu huanza kuhesabiwa kuazia huku hivyo tuwe makini saana kwenye swla hili, tuishie hapa kwa leo na nilipokosea basi Allah anisamehe na kunipa nguvu zaidi.
"FIKISHA YALIYOFIKISHWA"
"Wa aza Aslaam Alaykum Wa Rahma Tullah Wa Barakatuh"
Leo Bi Idhin Llah In Sha Allah tutaangalia Mambo(5) ambayo kwamba yanatengua Udhu kwa Mtu na kumfanya asiwe na Rukhsa ya ALLAH kuiendea SWALA.Twendeni pamoja.
- Ghuruj Shay'in min ahadil sabih layn.(yaani kutokwa na kitu kwenye moja kati ya njia/tupu mbili) hapa kinachomaanishwa ni kwamba ikiwa mmoja wetu ametokwa na haja kubwa ama ndogo basi Udhu wake utakuwa na mushkiri hadi pale atakapostanji(kutawadha/kujichamba).
- Naumi(Naumi ni usingizi hivyo ikiwa mtu amelala kisha akaamka basi yamlazimu kuchukuwa Udhu ili aendelee na Swala na hii ni kwa sababu wakati wa usingizi kuna mengi yanatokea ambayo hatuyajuwi wala kuyasikia.
- Zawa'alil Aqli.(kutokwa na Akili) bi maana kwamba ikiwa mmoja wetu hajielewi ama haelewi nini anafanya,mfano dhahili Mgonjwa wa akili basi huyu naye atakuwa hana Udhu.
- Lamsil maria'atil jinabiya.(kugusana na mwanamke ambae si haram kwako kumuoa, yaani huyu ni mwanamke ambae hauna nasaba/undugu nae, ila kama umegusana na dada,mama,shangazi na ndugu wengine basi hii haitenguwi Udhu na kwa wanawake ni kinyume chake.
- Mathil qubul awi dubul.(kugusa moja kati ya tupu mbili yaani ya mbele au nyuma hili pia hubatilisha Udhu na kumfanya mtu asiweze kuswali la sivyo akiswali ni sawa na kuwa anafanya mazoezi tu.
kwa maana ya kisharia(Dini) ni ibada ya kabla ya swala na baada ya twahara ambayo huambatinisha utiaji /uwekaji maji kwenye viungo vya mwili pamojana Dua.
Ndugu zangu Udhu ni jambo la kuzingatia sana maana hata Swawabu za swala zetu huanza kuhesabiwa kuazia huku hivyo tuwe makini saana kwenye swla hili, tuishie hapa kwa leo na nilipokosea basi Allah anisamehe na kunipa nguvu zaidi.
"FIKISHA YALIYOFIKISHWA"
"Wa aza Aslaam Alaykum Wa Rahma Tullah Wa Barakatuh"
Comments
Post a Comment