Hatua (5) za kufanya wakati unamlingania mtu.
Aslaam Alaykum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh ndugu zangu, naam hakika kwa uwezo wa ALLAH leo tunakutana tena na kama ilivyo ada kwa uchache wa shukran tuseme Alhamdulillah ikiwa tunamshukuru "ALLAH MTUKUFU MWINGI WA REHMA MWENYE KUREHEMU"Leo hii tutaangalia hatua ama vitu(5) vya kufanya wakati wa kumlingania mtu.
Naam:KULINGANIA-ni kitendo cha kumueleza mwana wa Adam kuhusu Dini tukufu ya UISLAM na faida zilizopo ndani yake, kwa maana nyingine tunaweza sema ni kumshawishi Mja arejee kwa Mola wake kupitia Dini tukufu ya UISLAAM.
Hivyo basi kwa kuwa ALLAH katuleta hapa Duniani kwa lengo kubwa la kulingania Dini yake kama vile walivyofanya Waja wema(Mitume&Manabii) basi nasi tulobakia tuendeleze jukumu hili kwa usahihi wake ikiwa kufuata hizi hatua(5).
- SALAAM,yaani "Aslaam Alaykum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh" hii ni salam ya kiislam ambayo kila aliye muislam anapaswa kumsalim aliye muislam mwenzake na kwa Manaswala(wasio waislam) kama vile ilivyoelekezwa.Vivyo hivyo endapo unahitaji kumlingania mtu basi ni vizuri ukaanza na salaam kwa maana hii humfanya mtu awe taari kukusikiliza kwa hekima zote.
- KUJITAMBULISHA,na baada ya salaam inampasa mwenye kulingania ajitambulishe kwa jina/majina yake kwa yule ambae anahitaji kumlingania na baada ya hapo tunaweza muuliza tunaetaka kumlingania pia ajitambulishe kama ilivyo kwaetu.
- KUUNGA UDUGU/UNDUGU,Kikubwa kinachomaanishwa ni kuwa unahitaji kutengeneza undugu ama urafiki ili muweze kuelewana.Maneno maarufu yanayozungumzwa ni(NAAM SASA NDUGU YANGU MFANO IBRAHIM, mimi na wewe ni ndugu na undugu wetu unaunganishwa na kalma tukufu"hapa tunatamka"SHAHADA"
- KUELEZEA UKUBWA ALLAH,baada hatua ya tatu kutamka shahada kinachofata ni kuelezea ukubwa wa ALLAH kwa kutaja sifa kuelezea sifa zake(yaani yale majina yake) ila kwa ufupi tuelezee sifa tatu muhim (.1).ALLAH NI KHALIQ, yaani ni muhumbaji hapa tuna uwezo wa kuvitaja vyote tunavyovijua Allah kaviumba ikiwemo binadam mwenyewe.(2)ALLAH NI MALIIK(yaani ni mwenye kumiliki hapa pia tunataja vitu vyote tuvijuavyo vinavyomilikiwa na ALLAH,mfano Uhai,Uzima,Utajiri,Umaskini,n.k.(3)AALAH NI RAZAQ(yaani ni mwenye kuruzuku/kutoa riziki hapa tunazungumzia riziki ambazo Allah anatoa kwa waja wake,mfano kipato/utajiri,n.k.
- TASHKIIR,naam baada ya kupitia hatua zote hizo nne hatimae hatua ya tano na ya mwisho ni Tashkiir yaani ni kumtaka anaelinganiwa ayafanyie kazi kwa vitendo yale aliyolinganiwa,na hapa mara nyingi tunasema"Hakika mafanikio ya bin adam hapa Duniani,Kaburini na Kesho Akhera ALLAH hajayaweka kwenye sifa zake wala sehem nyingine yoyote isipokuwa ni kwenye DINI kaamili na Dini kaamil ni kufuata maamrisho ya ALLAH(S.W) na kukatazika na MAKATAZO yake kupitia mafundisho sahihi ya Mtume Muhammad(S.A.W) na kwa maana hiyo basi tunaweza kumkaribisha anaelinganiwa Msikitini,Jawula na mambo mengine ya kiibada na kumuuliza kama yu tayari kufanya hivyo ila si lazima.
"FIKISHA YALIYO FIKISHWA"
"Wa azah Aslaam Alaykum Wa Rahmatullah Wabarakatuh"
Comments
Post a Comment