Nguzo(5) za Uislaam.
Aslaam 'Alaykum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh ndugu zangu katikan Iymaan,hakika leo kwa mara nyingine tena kwa uwezo wa Allah(S.W) tunakutana tena kwenye ukurasa wetu kujuzana amma kukumbushana mambo kazaa wa kazaa bi mana kwamba Binadam ni mwenye kughafirika.Kabla ya yote basi tumshukuru Allah(S.W) kwa kutuweka hadi leo hii Sha'aban 2/1438 sawa na 29/4/2017 huku tukiwa tunaukaribia mwezi wa Ramadan.Hivo basi kwa uchache wa shukuran basi tuseme ALHAMDULILLAH na kwa uwingi wake basi ni kutekeleza yale Allah aliyotuamrisha.Leo tutaenda angalia Nguzo tano za Uislam yaani vitu vitano muhimu vinavyofanya Uislaam uitwe hivi bi mana kwamba bila hivi vitu Uislaam hijakamilika, twendeni pamoja kwa Uwezo wa ALLAH.
"FIKISHA YALIYOFIKISHWA"
Wa azah Aslaam 'Alayjum Wa Rahmayullah Wa Barakatuh"
- Shahadul Llah,yaani kushuhudia kwa Allah ikiwa na maana kwamba kutamka shahada yaani(Ashahud Llah ilah ila Allah wa ashahadu anna Muhammad Rassulullah)Maana yake ni kwa nashuhudia hakuna Mwenyezi Mungu apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na Muhammad ni Mtume wake.,hii ni nguzo ya kwanza kabisa ya uislaam na ndiyo maana hata mtu akihitaji kusilimu basi lazima asemeshwe hii SHAHADA,na hata wakati wa mauti kama mmoja wetu akiweza kutamka Shahada hii basi Allah ampeleka peponi moja kwa moja.
- Iqamat Swalaa,.(kushikamana na swala) yaani kuswali haswa swala za Faradhi(swala 5) na Swala za Sunna pia,ndugu zangu swala ni kati ya msingi mkubwa wa muislam na ndiyo kinachotutofautisha sisi na Manaswala(Wasio waislaam) hata pia siku ya hesabu(Qiyama) basi cha kwanza kitachoangaliwa ni swala alafu Amal zinafuata.
- Itawu Dhakaa,(kutoa zakaa) ambayo hii hutolewa mara moja kwa mwaka ambayo huwa ni Eid Alhaj(Eid kubwa) ambayo kila muislam mtu mzima anatakiwa kuchinja mnyama au wanyama, lakini pia bila kusahau kutoa sadaka.
- Saum Ramadaan,(Kufunga Ramadaan ambayo inakuwa katika mwezi mtukfu wa Ramadaan na inakuwa siku 29-30,mwezi huu ni wenye fadhwira sana bi maana kwamba mwenye kufunga kwa usahihi wake anasamehewa makosa yake yote aliyoyafanya zamaani.
- Hiyjun Baytun limanstatwa,(Kuhenda kuhiji katika Nyumba tukufu(Msikiti) mtukufu wa Makka kwa mwenye uwezo,na hii inampasa mwenye kufanya hivyo afanye angalau mara moja katika uhai wake ili iwe sababu ya yeye kusamehewa makosa yake na ALLAH(S.W)
"FIKISHA YALIYOFIKISHWA"
Wa azah Aslaam 'Alayjum Wa Rahmayullah Wa Barakatuh"
Comments
Post a Comment