Historia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi :5

Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh ndugu zangu katika Iymaan naam katika mwendelezo wetu kuhusiana na Historia ya Mtume wetu Habeeb Muhammad(S.A.W)leo hi tunakutana tena.Na kabla ya yote basi tumshukuru ALLAH kwa kutupa afya hadi leo hii bi mana kwa kuna wengine wengi ALLAH kawaja'alia Mitihan mbalimbali.basi kwa uchache wa shukran tuseme ALHAMDULILLAH. 

Naam na leo hii tutaangalia baada ya Muhammad kutangaza Dini kwa wapinzani na yale yaliyomtokea  basi kilichofuata ni KUSUSIWA NA KUTAKA UKOO WAKE(BANU HASHIIM) UMUONDOE MAKKA.

BISMILLAH RAHMAN RAHIIM.
Naam na baada ya Makureishi kushindwa kumnyamazisha Mtume Muhammad kwa Vituko,Rushwa na Mateso basi waliamua  Ukoo wake wa Banu Hashiim umuondoe MAKKA lakini Banu Hashiim walikataa.

Baada ya hapo Mkaureishi waliwaamrisha Mtume Muhammad, Wafuasi wake na Ukoo wa Banu Hashiim watoke Makka na kwenda kuishi kwenye Mlima uitwao.Shuab Abu talib,Banu hashiim waliama Makka na kwenda kuishi huko kwa Miaka (3) huku wakipitia Mateso,Dhiki na Njaa na hata kula Mizizi pia walikosa nguo. 

Wakati huu wa kuishi katika Mlima wa Shuab Abu Talib Mtume Muhammad alipata msaada mkubwa kutoka kwa Mkewe Bi Khadija na Ami yake Abu Talib,lakini ALLAH aliwachukuwa hawa waja wake wawili(walifariki) na hapo ndipo Mtume Muhammad alibaki peke yake na hapo ndipo Makureishi walipozidisha mateso kwa Waislam.

MIRAJI-KUPELEKWA MBINGUNI KWA MTUME MUHAMMAD(S.A.W).
 Kabla ya  kwenda Madina Mtume Muhammad aliteremshiwa Jibril(A.S) na Mola wake ili aje kumchukua na ampeleke Mbinguni.Jibril alimchukua Mtume Muhammad toka Makka hadi Jerusalem ambako alikutana na Mitume iliyokuja Duniani kabla yake, akawaswalisha kisha akapaa Mbunguni kuoneshwa Nuru na Utukufu wa ALLAH.

Hii ilikuwa neema kubwa aliyopewa Muhammad na Mola wake na huko Mtume Muhammad alipewa "MSAMAHA"kwa wenye kutubia na kufanya Mema,pia alipewa Amri ya kiswali swala(5)  na ALLAH.

HIJRA-KUHAMIA MADINA KWA MTUME MUHAMMAD(S.A.W)
Ikiwa miaka(13) Muhamad baada ya kupewa Utume,Makureishi walipanga kumuuwa Mtume Muhammad,na hivyo walichagua wauwaji na kwenda kuizunguka nyumba ya Muhammad ili wafanikishe Adhma yao.Lakini ALLAH alimpa Muhammad udhihiri wa swala hili na hivyo Muhammad alimtaka Binam yake ALI IBN ABU TALIB,akalale kitandani kwake na kumuamuru arudishe Amana zoteza watu ambazo Mtume Muhammad alichukuwa.,

Usiku hule hule Mtume Muhammad alitoka Makka na rafiki yake kipenzi Abu Bakar na kwenda kujificha kwenye pango la  "THAUR"weengi tunalifaham kama pango la "JABAR HIRA"Makureishi walifika hadi nje ya pango lile lakini hawakuweza kugundua ndani kuna nini wakati kumbe humo ndimo walimo Muhammad na Abu Bakar.Abu Bakar alikuwa na hofu sana baada ya kuona Makureishi wapo nje ya pango lile lakini Mtume Muhammad akamtoa hofu.
"USIHUZUNIKE MOLLAH YU NASI"(Q:9:40)

Na hapo ndipo wakafanikiwa kuingia Madina bila kudhulika na Mwenyezi Mungu akaitaja Hijra hii katika Qur'an tukufu anasema.

"Na (kumbuka ewe Muhammad) wakati walipokufanyia hila wale waliokufuru,ili wakufunge au wakuuwe au wakutowe kwa hali mbaya katika Makka na kufanya hila zao hizo,na Mwenyezi Mungu ni Mboraa wa kupindua hila za(watu wahovu)"{Q:8:30}

Je ni vipi Maisha Mtume Muhammad yalikuwaje alipofika Madina,wenyeji waliwapokea vipi na mengine mengi usikose kutembelea Blog hii wakati mwingine tutakujuza.

"FIKISHA YALIYO FIKISHWA"
"Wa azah Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh"
 

Comments

Popular posts from this blog

Mitume 25 iliyotajwa kwenye QUR'AN.

Histotia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi :6

Historia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi:1