Historia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi :4
Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh ndugu zangu katika Iymaan,naam hakika kwa Rehma za Allah(S.W) ni siku nyingine tena tunakutana kujuzana machache kuhusiana na Historiya ya Mtume Muhammad(S.A.W).
Naam na leo tutaangalia ni vipi Mtume Muhammad alianza kutangaza DINI kwa wasio waislamu.
Mtume Muhammad alianza kutangaza DINI YA UISLAM YA ALLAH kwa wasio waislaam polepole na kwa siri kwa marafiki na jamaa zake kwa muda wa miaka(3) na watu waliosilim ndani ya mda huu walikuwa chini ya Thalathini.
Baadhi ya watu waliosilimu ndani ya muda huu ni.
Na baada ya miaka (3) hii ya kutangaza DINI ya ALLAH hapo ndipo ALLAH akamuamrisha Mtume wetu Kipenzi wa Darja aanze kutangaza DINI waziwazi bila kificho.
Na hapa sasa Mtume Muhammad alipanda juu ya Mlima Safa karibu na MAKKA na kutangaza kuwa
"Mwenyezi Mungu ni Mmoja "na akiwahasa Waarabu wa Makka juu ya azabu kali ya ALLAH kisha kuwataka waishi kutokana na Maamrisho ya ALLAH.
Suala hili liliwakwaza sana waarabu wa Makka kiasi cha kuamini kuwa watapoteza Enzi na Nguvu zao pamoja na Maslah wanayopata kutokana na Masanamu yaliyokuwemo ndani ya "KAABA"
Hapo ndipo Waarabu wa Makka walianza kumtisha Mtume Muhammad kuwa madhala makubwa yatamkuta endapo kama ataendelea kutangaza Dini hii Adhwiim ya ALLAH.Lakini Mtume Muhammad hakutingishika na katazo hilo.
Siku chache baadae Mtume Muhammada alikwenda kwenye "KAABA" na kutangaza kuwa "hapana Mola apasae kuhabudiwa kwa Haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na Muhammad ni Mjumbe wake". Washirikina walistaajabishwa sana na swala hili na kuuzika, hivyo walijaribu kumvutia Mtume Muhammad kwa Mali,Utukufu,Wanawake na hata kwa Ufalme lakini Mtume Muhammad aliwajibu"Ikiwa mtaniwekea Jua katika mkono wangu wa kulia na Mwezi katika mkono wangu wa kushoto,sitoacha jambo hili la kutangaza DINI ya ALLAH"
Hapa ndipo washirikina walianza kuwatesa Muhammad na wafuasi wake,baadhi ni kama Bilal,Ammar na Khabbab walitupwa juu ya michanga ya moto ya jangwani chini ya jua kali huku wakiwekewa mawe mazito juu ya vifua vyao,wengine waliburutwa njiani kwa kamba,wengine walipigwa vibaya bila ya huruma mpaka walifairiki.
Washirikina wa Kikureishi hawakuweza kumtesa sana Mtume Muhammad kutokana na Utukufu wa kabila lake la "BANU HASHIM" kwani kufanya hivyo kungeweza kuanzisha vita.Licha ya hivyo Muhammad alipata maudhiko kadhaa wa kadhaa kama kuwekewa miba na taka njiani,na mabo yalivyoharibika sana Mtume Muhammad alitoka Makka na kuamia "Taif"Mji karibu na Makka ili kutangaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu.
Nako pia alihujumiwa vibaya pia na kupigwa mawe na watu wa Taif,hadi alikaribia kuzimia, alikuwa amejawa na amaumivu na hivyo hakuwa na la kusema zaidi ya.
"Ewe Mola,waongoze njia sawa kwani wao hawafahamu neno"
Na kwa Muda wa miaka(5) kuteswa kwa Waislaam, Lakini watu walizidi kuingia kwenye Uislaam na kuacha Ushirikina.Mwaka wa(6) wa Mtume Muhammad, watu wawili muhim HAMZA&UMAR IBN KHATTAB walisilimu na kuwafanya wafuasi wa Mtume Muhammad kuwa na nguvu zaidi ya kuendelea kulingania DINI YA ALLAH.
Naam kwa leo tuishie hapa na In Sha ALLAH tukutane siku nyingine katika muendelezo wa Historiya hii Tamu na yenye kukuza Iymaan zetu.Nilipokosea basi ALLAH na nyie ndugu zangu katika Iymaan mnisameh na ALLAH anipe nguvu zaidi tuzidi kujuzana.
"FIKISHA YALIYOFIKISHWA"
"Wa azah Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh"

- Bi Khadija (R.A)
- Ali (K.W)Binamu na mtoto wa kumlea wa Mtume Muhammad(S.A.W).
- Zaiid,Mtumwa aliyeachiwa huru na Muhammad.
- Abu Bakar Sadiq(R.A)
- Uthman Ibin Affan(R.A)
- Talha.

Comments
Post a Comment