Historia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi:1
Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh ndugu zangu katika Iymaan,hakika leo ni siku nyingine tunakutana katika ukurasa wetu kama ilivyo ada kujuzana mambo mbalimbali yahusuyo Dini yetu Adhwiim ya UISLAAM,na leo hii kwa Idhin ALLAH tutaangalia Historia ya Mjumbe wa mwisho wa ALLAH kipenzi cha ALLAH, Kiigizo chema kwetu Mtume Muhammad(S.A.W),naamu twendeni pamoja In Sha Allah. Mtume Muhammad(S.A.W) alizaliwa Makka-Arabuni tareh 12-Rabbil Awwal(Mfungo sita) Miaka 54 BK.Sawa na 20(04) 570/571.B.I,Juma Tatu Alfajiri.Ndugu zangu kwenye swala la mwaka wa kuzaliwa kwake hapa kuna Maulamaa wametofautiana na ndiyo maana nimeweka miaka yoote miwili hapo. "Na sema ukweli umefika nauongo umetowekw/utaondoka,kwa hakkika uongo ni wenye kuondoka"( QUR'AN.17:81). Baba yake alikuwa akiitwa Abdallah(ikiwa na maana ya mja wa ALLAH) na alifariki miezi 6 kabla ya kuzaliwa kwa mwanae Muhammad,na ...