Histotia ya Mtume Muhammad(S.A.W) kwa Ufupi :6
Aslaam 'Alaykum wa Rahmatullah wa Barakatuh ndugu zangu katika Iymaan,naam Alhmadulillah kwa kuwa tunakutana tena leo hii kwenye muendelezo wa Historia ya Mtume Muhammad kwa uchache wake na tukiwa mwishoni mwa Mada yetu. BISMILLAH RAHMAN RAHIIM. MAPOKEZI YA MTUME MUHAMMAD NA ABU BAKAR SIDIQ KATIKA JAMII YA MADINA BAADA YA KUWASILI KWAO. Mtume Muhammad na Abu Bakar walipowasili Madina walipokelewa kwa shangwe na furaha na Waislam wa Madina kwani walikuwa na hamu kubwa ya kumuona Mtume wa Mwenyezi Mungu. Mtume Muhammad baada ya kufika Madina alimuachia Ngamia wake (HATAMU) ambae alikuwa anamtumia katika usafiri, na Ngamia huyu alienda kusimama katika kiwanja tupu cha ndugu wawili Mayatima na kuanza kula majani, na Mtume Muhammad aliamua kununua kiwanja kile na kujenga Msikiti na nyumba ndogo ya pembeni. Baadae Msikiti huu pamoja na nyumba ile vilikuwa sehemu ya kufikia wegeni(wasafiri) wasiokuwa na mahali pa kufikia, pia ilikuwa ni sehemu ya mikutano...